RESIPE ZA KIPWANI

Resipe ya Kachori 
Mahitaji
1. Viazi mviringo vikubwa vitano
2. Unga wa dengu robo
3. Pilipili  manga ya kusagwa kijiko kimoja cha chai
4. Rangi ya viazi kijiko kimoja cha chai
5. Bizari nyembamba ya kusagwa kijiko kimoja cha chai 
6. Dania fungu moja
7. Hoho moja kubwa
8. Karoti mbili
9.vitunguu maji vikubwa viwili 
10. Tangawizi mbichi
11. Kitunguu saumu punje tano
12. Limau
13. Uto robo
14. Chumvi kwaajili ya ladha

 Matayarisho
Vimenye/shambua maganda viazi, vikate kwa umbo la mramba kisha vioshe uvitie sufuriani pamoja na tangawizi na kitunguu saumu ulichokiponda kwa chumvi,ongezea maji vikombe viwili na ubandike viazi vyako jikoni

Viazi vikishaiva vitie pilipili manga,bizari nyembamba kisha vikamulie limau na uanze kuviponda kwa kutumia mwiko au mkono mpka vivurugike

Katakata vitunguu maji, hoho,dania na karoti vipande vidogo vidogo kisha changanya kwenye viazi ulivyoviponda,hakikisha mchanganyiko wako umechanganyika vizuri kisha weka kando

Chukua mchanganyiko wako wa viazi na viungo kisha anza kutengeneza viduara huku ukieka pembeni 

Chukua unga wa dengu uutie kwenye bakuli pamoja na rangi ya viazi, chumvi kwaajili ya ladha na maji.
 Anza kuukoroga unga wa dengu kwa kutumia kijiko,usiwe laini na wala usiwe mzito.

Tia mafuta ya uto kwenye karai na ubandike jikoni halafu chovya vidonge vya viazi kwenye unga wa dengu huku ukichoma kwenye mafuta  yaliyopata moto vizuri, moto uwe wa wastani ili kachori zako ziive kwa rangi ya kupendeza.

Unaeza kundaa kachori zako kwa chatini au ukwaju pamoja na pilipili ya maembe😋

Comments

  1. Nishaanza kuumia mapua ju ya harufu tamu ya food

    ReplyDelete
  2. Wow..... So yummy Mashaallah👌

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Aaah wapi😄😄😄kuandaa kitu moyo inapenda kuna kazi gani😄😄

      Delete
  4. Replies
    1. Kwanza wewe mtu wa kupenda viazi ....try this na hutojutia😋👌

      Delete
  5. Aaai jamani kwa kweli nitajaribu

    ReplyDelete
  6. Wow ‼️‼️‼️‼️ it looks nice

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TOXIC RELATIONSHIPS AMONG CAMPUS STUDENTS