KUFA KIOFISI, TAI SHINGONI

Ukatili wa kijinsia (wanaume)
Picha kutoka: freepik.com

Ukatili wa kijinsia ni nini? Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho kinaweza kusabisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na kutishiwa maisha, kunyimwa uhuru iwe hadharani au kwa kificho.

Mara nyingi kwenye harakati za kupinga ukatili wa kijinsia, wanaume hawapendi kuhusika moja kwa moja,wapo wanaosema hawanyanyasiki lakini ukweli ni kwamba hata wao wamo.

Kulingana na utafiti uliofanywa na muungano  wa Maendeleo ya wanaume,mwaka wa 2008, ripoti inaonesha kwamba Takriban wanaume milioni 2.1 nchi Kenya wamekuwa wakinyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya ukatili kila uchao, huku wengi wao wakiamua kubaki kimya kitendo ambacho kinawapelekea kuathirika zaidi kisaikolojia.

Hofu ikiwa ni moja wapo ya sababu inayomfanya mwanamume kunyamazia anayoyapitia na kuumia ndani kwa ndani haswa ikiwa unyanyasaji unaomkabili ni wa kimapenzi kwani inachukuliwa kama kitu cha aibu katika jamii.

Sababu Nyengine ikiwa ni dhana kwamba mwanamume hapigwi na mwanamke hii humfanya mwanamume kushindwa kuelezea anayopitia kutoka kwa mwenza wake kwa kuhofia kuonekana dhaifu mbele ya jamii.

Kuna baadhi ya jamii ambazo wanawake husifika katika kunyanyasa wanaume. Hili si jambo la kufurahisha kuwa "nyinyi" watu fulani ni mabingwa wa matusi, kusuta na kudhalilisha wanaume.

Wapo baadhi ya wanawake  wanaowaambia waume au wapenzi wao kuwa hawana kitu na kuwakejeli " mwanamume suruali" tena mbele za watu au watoto wao, maneno hayo ni unyanyasaji wa kijinsia na huwaumiza wanaume kisaikolojia na kimwili.

Visa kama hivi humpelekea mwanamume kujiua au hata kuikimbia familia yake kama njia moja wapo ya kuidhibithi hali yake na maumivu, na hapo ndipo mwanamke hujitokeza na kulalamika kwamba mume amemtelekeza na watoto. 

Kwa Muhtasari zaidi, ni vyema kufunguka na kueleza matatizo yanayokukabili ili kupata ushauri nasaha, lakini  pia jamii inafaa kutambua kuwa unyanyasaji unahusisha kila mtu, kila jinsia na hata mwanamume ni mhanga wa ukatili wa kijinsia

Reference 
1.The Star newspaper 6th April 2021
2. Ippmedia.com


Comments

  1. nice work...can't remember the last time I wrote a whole blog in Swahili this is a good challenge though.....

    ReplyDelete
  2. Nakala safi yenye maelezo na maelekezo kuntu. Zidisha.

    ReplyDelete
  3. Mashallah ,, nakala safi yenye maelezo mbashara ... Heko mrembo

    ReplyDelete
  4. Wanaume wengi wanazidi kuficha wanayoyapitia katika ndoa zao.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TOXIC RELATIONSHIPS AMONG CAMPUS STUDENTS

RESIPE ZA KIPWANI