SAMAKI MKUNJE, ANGALI MBICHI
Malezi
picha kutoka: unsplash free images
Malezi ni mchakato wa wamaandalizi ya Mtoto utakaomwezesha kukua, kukubalika na kushiriki katika shughuli za kijamii na kiutamaduni kwa kumlinda, kumjamiisha na kumpatia mahitaji na huduma za msingi.
Iwapo malezi ni mchakato wa wamaandalizi ya mtoto basi sharti iwepo mipango toka kwa wazazi ili kufanikisha hili.
Katika karne hii idadi kubwa ya wazazi wametelekeza wajibu wao, mfumo wa kidijitali umewafanya kuyaelekeza malezi ya watoto wao kwa watu baki nikiashiria wafanyi kazi wa ndani.
Mzazi anathamini simu au kipakatalishi katika muda wake wa mapumziko kuliko kukaa chini na mwanawe na ndio maana visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa watoto wadogo nimekuwa vikishughudiwa kila uchao.
Mwaka jana (2021) visa vya wanafunzi kuchoma majengo ya shule vilikuwa vikigonga vichwa vya habari huku vikiacha maswali ya nani wa kulaumiwa. Siku zote nyumba huanza kwa msingi na mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi, mtoto huanza kufunzwa nidhamu akiwa nyumbani kabla ya kupelekwa shuleni, haiwezakani mtoto mwenye nidhamu kuchukua hatua ya kuharibu majengo ya shule.
Fauka ya hayo, vijana wadogo ambao taifa limeelekeza macho kwao kama viongozi wa kesho, wamekua wakipoteza maisha yao katika mashambulizi kati yao na polisi kwasababu ya kujihusisha na makundi haramu, mfano; wakali kwanza.
Vilevile visa vya watoto kudhulumiwa na wafanyikazi vimekuwa vikiripotiwa kila uchao, yote sababu mzazi hana muda wa kuratibu mienendo ya mwanawe na kumhakikishia usalama.
Ni wajib na jukumu la kila mzazi kujua mwanawe atavaa nini, atakula nini, ataenda vipi shule na atarudishwa na nani nyumbani.
Bila shaka wahenga waliponena ya kwamba uchungu wa mwana ajuae ni mzazi hawakukosea na walilenga mahusiano endelevu kati ya mzazi na mtoto katika kipindi chote cha maisha yake.
Reference
1. https://malezi.sematanzania.org
๐๐
ReplyDelete๐
ReplyDelete๐ฏ kweli kabisa
ReplyDeleteKweli kabisa๐ฏ
ReplyDelete๐
ReplyDeleteUkweli mtupu
ReplyDeletesafi kabisaa .
ReplyDeleteUshasema aisee !✌️
ReplyDeleteWow ukwel mthupu...
ReplyDeleteYeah it's true
ReplyDeleteSawa kabisa
ReplyDeleteNi kweli
ReplyDelete๐
ReplyDelete๐ฏ
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteUkweli
ReplyDeleteKabisaa
ReplyDeleteNzuri
ReplyDeleteWise ๐ค๐พ๐ฅ
ReplyDeleteYeah that true
ReplyDeletePerfect broo
ReplyDeletePerfect
ReplyDeleteSure๐๐
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDelete