RESIPE ZA KIPWANI
Resipe ya Kachori Mahitaji 1. Viazi mviringo vikubwa vitano 2. Unga wa dengu robo 3. Pilipili manga ya kusagwa kijiko kimoja cha chai 4. Rangi ya viazi kijiko kimoja cha chai 5. Bizari nyembamba ya kusagwa kijiko kimoja cha chai 6. Dania fungu moja 7. Hoho moja kubwa 8. Karoti mbili 9.vitunguu maji vikubwa viwili 10. Tangawizi mbichi 11. Kitunguu saumu punje tano 12. Limau 13. Uto robo 14. Chumvi kwaajili ya ladha Matayarisho Vimenye/shambua maganda viazi, vikate kwa umbo la mramba kisha vioshe uvitie sufuriani pamoja na tangawizi na kitunguu saumu ulichokiponda kwa chumvi,ongezea maji vikombe viwili na ubandike viazi vyako jikoni Viazi vikishaiva vitie pilipili manga,bizari nyembamba kisha vikamulie limau na uanze kuviponda kwa kutumia mwiko au mkono mpka vivurugike Katakata vitunguu maji, hoho,dania na karoti vipande vidogo vidogo kisha changanya kwenye viazi ulivyoviponda,hakikisha mchanganyiko wako umechanganyika vizuri kisha weka kando Chu...