Posts

Showing posts from March, 2022

SAMAKI MKUNJE, ANGALI MBICHI

Image
Malezi picha kutoka: unsplash free images Malezi ni mchakato  wa wamaandalizi ya Mtoto utakaomwezesha kukua, kukubalika na kushiriki katika shughuli za kijamii na kiutamaduni kwa kumlinda, kumjamiisha na kumpatia mahitaji na huduma za msingi. Iwapo malezi ni mchakato wa wamaandalizi ya mtoto basi sharti iwepo mipango toka kwa wazazi ili kufanikisha hili. Katika karne hii idadi kubwa ya wazazi wametelekeza wajibu wao, mfumo wa kidijitali umewafanya kuyaelekeza malezi ya watoto wao kwa watu baki nikiashiria wafanyi kazi wa ndani. Mzazi anathamini simu au kipakatalishi katika muda wake wa mapumziko kuliko kukaa chini na mwanawe na ndio maana visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa watoto wadogo nimekuwa vikishughudiwa kila uchao. Mwaka jana (2021) visa vya wanafunzi kuchoma majengo ya shule vilikuwa vikigonga vichwa vya habari huku  vikiacha maswali ya nani wa kulaumiwa. Siku zote nyumba huanza kwa msingi na mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi, mtoto huanza kufunzwa ni...

MWANAMKE DEBENI!!!

Image
Mwanamke na uongozi  picha Kutoka :vectorstock Huku wananchi wakijiandaa kutimiza haki yao ya kimsingi ya kupiga kura mnamo mwezi wa Agosti  mwaka huu, kulingana na kifungu cha sheria 38(2) katika katiba ya Kenya 2010,           Kila mwananchi mtu mzima ana haki ya kushiriki uchaguzi huru wa haki na kumchangua kiongozi amtakaye. Maswali yameibuka miongoni mwa wananchi haswa kutoka kanda ya pwani, wakiuliza kama wanawake watajitokeza kwa wingi kuwania uongozi wa ngazi ya juu kama ugavana na urais licha ya kuwa katiba imewapa nafasi hiyo katika sura ya nne, kifungu cha sheria 27(3),                Wanawake na wanaume wana haki ya kushughulikiwa kwa usawa ikiwemo haki ya kupata nafasi sawa katika shughuli ya kisiasa. Kulingana na takwimu, wanawake wachache wametangaza rasmi kuwania kiti cha ugavana katika ukanda wa pwani, miongoni mwao ni pamoja na; Bi Aisha Jumwa kaunti ya Kilifi, Bi Umrah Omar kau...

KUFA KIOFISI, TAI SHINGONI

Image
Ukatili wa kijinsia (wanaume) Picha kutoka: freepik.com Ukatili wa kijinsia ni nini? Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho kinaweza kusabisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na kutishiwa maisha, kunyimwa uhuru iwe hadharani au kwa kificho. Mara nyingi kwenye harakati za kupinga ukatili wa kijinsia, wanaume hawapendi kuhusika moja kwa moja,wapo wanaosema hawanyanyasiki lakini ukweli ni kwamba hata wao wamo. Kulingana na utafiti uliofanywa na muungano  wa Maendeleo ya wanaume,mwaka wa 2008, ripoti inaonesha kwamba Takriban wanaume milioni 2.1 nchi Kenya wamekuwa wakinyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya ukatili kila uchao, huku wengi wao wakiamua kubaki kimya kitendo ambacho kinawapelekea kuathirika zaidi kisaikolojia. Hofu ikiwa ni moja wapo ya sababu inayomfanya mwanamume kunyamazia anayoyapitia na kuumia ndani kwa ndani haswa ikiwa unyanyasaji unaomkabili ni wa kimapenzi kwani inachukuliwa kama kitu cha aibu kat...