MWANAMKE DEBENI!!!
Mwanamke na uongozi
Huku wananchi wakijiandaa kutimiza haki yao ya kimsingi ya kupiga kura mnamo mwezi wa Agosti mwaka huu, kulingana na kifungu cha sheria 38(2) katika katiba ya Kenya 2010,
Kila mwananchi mtu mzima ana haki ya kushiriki uchaguzi huru wa haki na kumchangua kiongozi amtakaye.
Maswali yameibuka miongoni mwa wananchi haswa kutoka kanda ya pwani, wakiuliza kama wanawake watajitokeza kwa wingi kuwania uongozi wa ngazi ya juu kama ugavana na urais licha ya kuwa katiba imewapa nafasi hiyo katika sura ya nne, kifungu cha sheria 27(3),
Wanawake na wanaume wana haki ya kushughulikiwa kwa usawa ikiwemo haki ya kupata nafasi sawa katika shughuli ya kisiasa.
Kulingana na takwimu, wanawake wachache wametangaza rasmi kuwania kiti cha ugavana katika ukanda wa pwani, miongoni mwao ni pamoja na; Bi Aisha Jumwa kaunti ya Kilifi, Bi Umrah Omar kaunti ya Lamu, Kwale ni Bi Fathma Achani, Bi patience Nyange na Rachel Mwakazi kaunti ya Taita Taveta. Kaunti ya Tana river na Mombasa kufikia sasa hakuna mwanamke aliyejitokeza kuwania kiti hicho.
Katika mahojiano na baadhi ya wananchi katika mji wa Mombasa, wengi wamedai baadhi ya sababu zinazowafanya wanawake wasijitokeze kwa wingi kuwania vyeo vya ngazi ya juu katika uongozi wa kisiasa haswa katika ukanda wa pwani ni kama zifuatavyo:
1. Ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa wanawake wenzako, wakiongezea kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake.
2. Ukosefu wa fedha za kujihusisha na mchakato mzima wa kampeni.
3. Kasumba miongoni mwa wanaume kwamba hawaezi kuongozwa na wanawake
4. Kukosa uzoefu katika suala zima la uongozi.
5. Mila na desturi zinazopinga uongozi kwa wanawake.
Mwanamke zinduka wakati ni sasa!!Mila na tamaduni za kizamani zisikufunge kiasi ya kwamba ukakosa kutimiza malengo yako, zamani ilikua nadra kwa mwanamke kupelekwa shuleni kusoma ila sasa ni tofauti na hivyo basi kama unaeza kuingia darasani ukasoma na uongozi pia unauweza, na kama unaeza kuiongoza nyumba yako pale nyumbani kumshuhulikia mume wako na watoto ipasavyo basi hata wananchi unaeza kuwatumikia ipasavyo.
2022 nitakuwa kiongozi 😁😁
ReplyDeleteInteresting read..yes we can
ReplyDeleteNice one
ReplyDeletesafi kabisaa.
ReplyDeleteWanawake tuwakee😂✌️
ReplyDeleteHaki kwa kila jinsia
ReplyDeleteIko poa siz .. good work
ReplyDeleteSwadakta kabisa
ReplyDeleteBarabara kabisa
ReplyDeleteSadakta
ReplyDeleteSwadakta
ReplyDeleteNice 👍
ReplyDeleteGreat work 🥳
ReplyDeleteKabisa
ReplyDeleteNice one
ReplyDelete