SAMAKI MKUNJE, ANGALI MBICHI
Malezi picha kutoka: unsplash free images Malezi ni mchakato wa wamaandalizi ya Mtoto utakaomwezesha kukua, kukubalika na kushiriki katika shughuli za kijamii na kiutamaduni kwa kumlinda, kumjamiisha na kumpatia mahitaji na huduma za msingi. Iwapo malezi ni mchakato wa wamaandalizi ya mtoto basi sharti iwepo mipango toka kwa wazazi ili kufanikisha hili. Katika karne hii idadi kubwa ya wazazi wametelekeza wajibu wao, mfumo wa kidijitali umewafanya kuyaelekeza malezi ya watoto wao kwa watu baki nikiashiria wafanyi kazi wa ndani. Mzazi anathamini simu au kipakatalishi katika muda wake wa mapumziko kuliko kukaa chini na mwanawe na ndio maana visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa watoto wadogo nimekuwa vikishughudiwa kila uchao. Mwaka jana (2021) visa vya wanafunzi kuchoma majengo ya shule vilikuwa vikigonga vichwa vya habari huku vikiacha maswali ya nani wa kulaumiwa. Siku zote nyumba huanza kwa msingi na mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi, mtoto huanza kufunzwa ni...